Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi za jamii Tanzania,TANAPA,Alan
Kijazi akizungumza jambo wakati kamati ya Bunge ya ardhi,maliasili na
mazingira ilipotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira
wakifuatilia maelezo ya mkurugenzi mkuu wa TANAPA(hayupo picani).
Naibu waziri wa maliasili na Utalii,Mahamud Mgimwa akizungumza mbele
ya kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea hifadhi ya
taifa ya mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro ,Erasimus
Lufunguro akitoa maelezo kuhusu nusu maili katika mlima Kilimanjaro
kwa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea hifadhi ya
taifa ya mlima Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,maliasili na Mazingira,Mh James
Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokutana na maofisa wa
TANAPA na KINAPA katika ofisi za Hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Mjumbe wa kamati ya Ardhi ,maliasili na Mazingira,Suzan Kiwanga
akichangia jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea hifadhi ya taifa ya
mlima Kilimanjaro.
Eneo la nusu maili katika mlima kilimanjaro ambalo zamani lilitumiwa
na wakazi walioko jirani na eneo hilo kwa shughuli za kukata Nyasi na
badala yake walikata miti kabla ya kurejeshwa katika hifadhi ya taifa
ya KINAPA kwa ajili ya usimamizi ambapo hifadhi sasa limeanza kurejea
katika hali yake baada ya miti kuoteshwa.
Mjumbe wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Lekule Laizer
akizungumza jambo mbele ya wajumbe wenzake na naibu waziri wa
maliasili na utalii,Mahamud Mgimwa.
Wajumbe wa kamati wakiwa katika eneo la Nusu maili katika mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi mkuu TANAPA ,Alan Kijazi akiwa na mhifadhi mkuu wa KINAPA
Erasimus Rufunguro wakisilikiza kwa makini jambo kutoka kwa mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira,Mh James Lembeli(hayupo
pichani).
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira,James Lembeli
akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea hifadhi ya mlima
Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi maliasili na mazingira,James Lembeli
akimsadia kumbebesha mzigo wa kuni mmoja wa wakazi wanaoishi jirani na
mlima Kilimanjaro aliyekuwa akiokota kuni katika eneo la nusu maili.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Post a Comment