Home » » MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UWAKILISHI JIMBO LA KIEMBESAMAKI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UWAKILISHI JIMBO LA KIEMBESAMAKI

Written By JAK on Monday, February 3, 2014 | 6:34 AM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimchagua kwa siri mgombea wa Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo wa Mwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo mjini Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitumbukiza kura yake ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika jana asubuhi mjini Zanzibar. . Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Kituo chake cha kupigia Kura, kwa ajili ya kushiriki kupiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo, uliofanyika jana mjini Zanzibar leo asubuhi. Kushoto ni Mgombea wa Jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita 


Baadhi ya Wananchi wakisoma ubao wa matangazo kutafuta eneo walilopangiwa kupigia kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa zoezi hilo lililofanyika jana asubuhi mjini Zanzibar. Picha na OMR 
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger