Home » » MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MUASISI WA SHIRIKA LA AFYA NA ELIMU MIKOCHENI

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MUASISI WA SHIRIKA LA AFYA NA ELIMU MIKOCHENI

Written By JAK on Thursday, February 6, 2014 | 6:14 AM

Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu (MMHEN) liliyopo Mikocheni, Regent Estate, Dar es Salaam, anapenda kuutangazia umma kuwa tarehe 06/02/2014 kuanzia saa 02:00 asubuhi Shirika, pamoja na Taasisi zake zikijumuisha Kairuki Hospital (KH), Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) na Mikocheni School of Nursing (MSN) wataadhimisha miaka 15 ya kutokwa na muasisi wa MMHEN na Taasisi zake PROF. HUBERT CLEMENCE MWOMBEKI KAIRUKI .

Katika kuadhimisha siku hiyo, MMHEN na taasisi zake zilizo chini ya zitatoa huduma ya afya bila malipo kwa jamii pamoja na uchangiaji wa damu kwa hiari kwa ushirikiano wa BLOODAT na DAMU SALAMA itakayotolewa katika viwanja vya shule ya msingi Mikocheni kwa muda wa siku mbili (2) kuanzia tarehe 05/01/2014 hadi 06/02/2014. Shughuli hizi zitafuatiwa na mada (public lecture) itakayotolewa na Dr. Kaushik Ramahiya kutoka Hindu Mandal Hospital kuanzia saa 8:30 mchana ukumbi wa mihadhara , ghorofa ya tano hapo HKMU.

Pamoja na kutoa huduma ya afya bila malipo, Mwenyekiti wa MMHEN pia atakabidhi jengo la madarasa manne (4), ambalo limekarabatiwa na Kairuki Hospitali, vifaa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya shule pamoja na msaada kwa wahanga wa maafa ya mafuriko yaliyotokea Dumila mkoani Morogoro, hivi karibuni.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na : Gerlad Manongi manongiss@yahoo.co.uk 0715 847 444 or 2700021-4 : Arafa Juba 0715 289 264 arafamody@yahoo.com E-mail : info@kairukihospital.org Website: www.kairukihospital.org
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger