Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa
Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa utekelezaji wa
mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa kufuatilia na kutathimini
utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu,
Maji, Nishati , Uchukuzi na Utafutaji wa Rasilimali).
Mfumo wa BRN unaweka
wazi malengo pamoja na kuainisha uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi
katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.
Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia
Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa karibu
sana na OR-UUM.
Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji
wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi
ambazo huwasilishwa OR-UUM.
Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye
mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering
Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja
na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mikutano hii inalenga kutatua changamoto
Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia
Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja
na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza
Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo
makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana
ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa.
BRN
inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote
Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi ambayo
italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji.
Ili kuhamasisha ushiriki wa
sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha mfumo na taratibu za
ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba
sekta binfasi inatoa mchango wake stahiki katika kutekeleza BRN
Post a Comment