Home » » SIMBA YAVUTWA SHATI NA MTIBWA SUGAR,YATOKA SARE YA BAO 1-1 MJINI MOROGORO

SIMBA YAVUTWA SHATI NA MTIBWA SUGAR,YATOKA SARE YA BAO 1-1 MJINI MOROGORO

Written By JAK on Thursday, February 6, 2014 | 6:17 AM

Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba 
 Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa 
Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
 Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.
 Kipa wa Mtibwa Hasani  Sharifu  
 Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo
 Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.
 Simba wakishangilia Goli lao lilofungwa na Khamis Tambwe Bao lililofungwa dakika 50 ya mchezo.

Mpira Umemalizika Mtibwa 1 -1 Simba. Goli la Mtibwa Sugar Lilifungwa dakika ya 18 ya Mchezo bao Lililofungwa na Mussa Mgosi .Hadi Mapumziko Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa Goli Hilo Moja.Kipindi cha Pili Mpira ulianza kwa kasi Simba walishambulia Lango la Mtibwa mara kwa mara Na kujipatia bao la Kusawazisha katika dakika ya 50 ya Mchezo.Katika Mchezo Mchezaji wa Mtibwa Shaban Nditi Alionyeshwa kadi Nyekundu Dakika ya 69 baada ya Kutoa maneno Machafu kwa Mwamuzi.Dakika ya 72 Said Ndemla anaingia Kuchukua nafasi ya  Haruna Shamte,Dakika ya 75, Juma Mpakala Aliingia Kuchukua nafasi ya  Jamal Mnyate. Dakika ya 87  wanafanya mabadiliko ya mwisho, aliingia Abdallah Salum Kuchukua nafasi  Mgosi..
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger