Moja ya mabango yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru nchini. Hafla hii ilifanyika muda mfupi kabla Rais Kikwete hajapanda ndege kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kupanga mikakati ya kupambana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na faru.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud Mgimwa.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Far baada ya kuyazindua rasmi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Farubaada ya kuyazindua rasmi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk. Mahamoud Mgimwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadick.
Post a Comment