Home » » MGIMWA AWAOMBA WANANCHI KUMKOPESHA IMANI YAO ILI NAYE AWALIPE KWA KUWATUMIKIA KULETA MAENDELEO.

MGIMWA AWAOMBA WANANCHI KUMKOPESHA IMANI YAO ILI NAYE AWALIPE KWA KUWATUMIKIA KULETA MAENDELEO.

Written By JAK on Friday, March 14, 2014 | 8:58 AM





Wananchi wa kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama,Iringa Vijijini wakinyanyua mikono yao juu kumuunga mkono Mgombea Ubunge jimbo la kalenga,Ndugu. Godfrey Mgimwa.Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16 siku ya jumapili.

 Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili kuzisikiliza sera za mgombea Ubunge wa Jimbo la kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika kwenye kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama Iringa Vijijini

 Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama Iringa vijijini, akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani yao na kumpa kura za ndiyo siku ya Machi 16,Jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo katika jimbo hilo.

Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis Lupala akipiga magoti kumuombea kura kwa wananchi mgombea Ubunge wa CCM Bw. Godfrey Mgimwa.

Baadhi ya Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger