Home » » Mama.Samia Suluhu Hassan achaguliwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba

Mama.Samia Suluhu Hassan achaguliwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba

Written By JAK on Friday, March 14, 2014 | 8:50 AM

Hatimaye  Bunge maalum la Katiba limemchagua Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wake mjini Dodoma.


Hii inakuja baada ya  kumchagua Mhe.Samweli Sitta kuwa Mwenyekiti. Mhe Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour. Kura 7 ziliharibika .


 Katibu wa Bunge hilo Maalum ambaye atajulikana wakati wowote kuanzia sasa ataapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ijumaa asubuhi Ikulu ndogo Dodoma.


 Katibu wa Bunge ndiye atakayemwapisha Mwenyekiti na Makamu wake, na Mwenyekiti atawaapisha wajumbe wote, ndipo shughuli itapoanza rasmi ya kuandika katiba mpya.



Mhe.Samia Suluhu  Hassan (anaye angalia kamera)akipongezwa na aliyekuwa mshindani wake Mhe Amina Abdalla Amour  mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Maalum la Katiba mteule Dodoma, akishukuru wajumbe kwa kumchagua 

Wajumbe kinamama wakishangilia mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kumpata Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma leo

Hoi hoi na nderemo

Chereko chereko...


Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Dodoma
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger