Home » » RIDHIWANI KIKWETE ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE

RIDHIWANI KIKWETE ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE

Written By JAK on Friday, March 14, 2014 | 9:34 AM


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.

Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.




===========  ======== ======


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze

kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,  Ndugu Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya

kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.



Akisindikizwa na washindani wake

katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ndugu Ramadhan Maneno, pamoja na Ndugu Imani Madega, 

Ridhiwani aliwashukuru wana CCM na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa

kumuunga mkono.



Ridhiwani pia ameahidi kushirikiana na

wana-Chalinze katika kutekeleza yote yaliyofanywa na wabunge waliotangulia

lakini pia amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa

Chadema inayodhihaki kuwa yeye sio mkazi wa Chalinze.



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze

kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi

kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo hilo.



Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia

wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa wagombea kutangaza sera

zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa

Chalinze.



Alisema kuwa

hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kurumbana na

kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa.



Alisema

hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa

tangia mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia

wananchi.



Alisema kuwa

kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji ya uhakika,

kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi wa maji ya uhakika.



Aliongeza kuwa

pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya za uhakika za afya kwa

wakazi wa eneo la Chalinze. "Najua

awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna

ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo

yanaongezeka"alisema Ridhwani.



Aliongeza kuwa

ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma mbalimbali kama hizo

za za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo.



"Watu

wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa. Hapana! Yaani tena hata

sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura

huku sio! Ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni

wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa hapa Chalinze"alisema Ridhiwani.



Kuhusiana na

tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo jukumu

kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu

imekuwa ikifanya hivyo. Alisema kuwa

atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu baina ya

wafugaji na wakulima.



Ndugu Ridhwani

anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. Uchaguzi mdogo

wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo

Said Bwamdogo.


Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger