Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi (CCM),Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na mmoja wa
wanakijiji,mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni wa uchaguzi
mdogo wa jimbo hilo,uliofanyika katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa
Vijijini,huku kukiwa na mvua kubwa ikinyesha,ambayo hata hivyo haikuzuia
kufanyika kwa mkutano huo.Wananchi wa Kijiji hicho walionekana kuw ana shauku
kubwa ya kutaka kumsikiliza Mgombea huyo bila kujali kulowana na mvua.Uchaguzi
unatarajiwa kufanyika Machi 16.
Wanakijiji cha Wenda
wakimpungia Mgombea Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,huku
shangwe na vifijo vikiwa vimetawala eneo hilo pasina kujali mvua kubwa
ilioyokuwa ikiendelea kunyesha eneno hilo.
Pamoja na Mvua kubwa
iliyokuwa inanyesha katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa
Vijijini,wanakijiji wa eneo hilo walionekana kuvutiwa mno na sera za mgombea
ubunge wa CCM,Godfrey Mgimwa alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara wa
kampeni.Kama uonavyo pichani baadhi ya Wanakijiji wakilikimbiza gari ya mgombea
huyo mara baada ya kumaliza mkutano wake.Mgombea huyo aliwaomba wampigie kura
za ndio na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge wa jimbo hilo,ili wayamalizie
yale yaliyokuwa yameachwa na Mbunge aliyekuwepo hapo awali,Marehemu Dk Willliam
Mgimwa.
Post a Comment