Home » » MVUA DAR YASABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA MABOMBA YA MAJI JANGWANI

MVUA DAR YASABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA MABOMBA YA MAJI JANGWANI

Written By JAK on Wednesday, April 16, 2014 | 5:31 AM




Mabomba yaliathirika baada ya mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki eneo la Jangwani.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa  DAWASCO, Jackson Midala (wa kwanza kushoto) walipotembelea eneo la Jangwani,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindokoleo ametembelea eneo la Jangwani, Darajani, barabara ya Morogoro kujionea uharibifu mkubwa wa mabomba ya maji.

Mabomba hayo ya inchi 16 yenye urefu wa mita 12 yamezolewa na maji kutokana na atharii liyoletwa na mvua kubwa ya mwishoni mwa wiki inayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Ni athari kubwa ambayo imesababishwa na mvua hii na mpaka kukata mabomba ya maji, ni muda mrefu tangu mvua ya aina hii kutokea Dar es Salaam”, alisema Inj. Mrindoko.

“Nimekuja kuangalia hali halisi na kuona namna gani tutafanya kufanya ukarabati wa mabo mba haya, ili kurudisha huduma ya maji kwa maeneo yaliyoathirika baada ya tukio hili. Tumefanya tathmini na kuona nini cha kufanya na utekelezaji utaanza mara moja”, aliongeza Inj. Mrindoko.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger