KINANA AFANYA MKUTANO WA HADHARA NA WANANCHI WA NAKAPANYA WILAYANI TUNDURU MKOANI RUVUMA,AWAHIDI KUMALIZA TATIZO LA BEI YA KOROSHO.

Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitolea ufafanuzi wa kina kwa Wakazi wa kijiji
cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma mapema leo jioni,kuhusiana na
tatizo sugu la bei ya zao la Korosho kwa wakulima,ambao wamekuwa wakilalamika
kwa muda mrefu,Kinana aliwahakikishia Wanachi hao kuwa tatizo hilo watalifanyia
kazi ipasavyo na kufikia hatua ya kulimaliza kabisa.
Aidha tatizo hilo ni kubwa kwa upande wa mikoa ya
Kusini,ikiwemo Mtwara,Lindi na Ruvuma.Kinana alibainisha kuwa CCM kitahakikisha
suala la hilo linashughulikiwa kwa umakini
mkubwa ikishirikiana na Serikali sambamba na sambamba na taasisi
zinazohusika na zao hilo,ili kukomboa uchumi wa Wananchi wa eneo hilo hasa kwa
kuhakikisha viwanda vya kubangua korosho vinajengwa na vile ambavyo
vimebinafsishwa na havifanyi kazi kunaandaliwa utaratibu ambao utawafanya
wawekezaji wengine kupewa ili vifanye kazi na kutatua tatizo la bei ndogo ya
zao hilo inayolipwa na wanunuzi.
Katika ziara hiyo hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC
siasa,Itikadi na uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dkt.AshaRose Migiro.

Baadhi ya Wakazi wa
kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakishangilia jambo mara
baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,kuzungumzia na kufafanua
vyema kuhusiana na tatizo kubwa lililopo kwenye zao la Korosho,ambako
kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwemo suala la bei ya
ununuzi wa Korosho kuwa ndogo,malipo kutokulipwa kwa wakati kwa wakulima na mengineyo.

Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ,Mh.Ramo Matalla Makani
akielezea baadhi ya matatizo yanayoisumbua Wilaya hiyo kwa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana (pichani kulia) mapema
leo,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nakapanya,Wilayani
Tunduru mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake wataanza ziara yao rasmi leoo
Wilayani humo mkoani Ruvuma kwa madhumuni ya kuimarisha chama na kukagua miradi
ya maendeleo inayotekelezwa kwa Ilani ya CCM,katika Mikoa ya Ruvuma na Mbeya.


Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru
mkoani Ruvuma wakiwa wamekusanyika mapema jana wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na ufumbuzi wa
matatizo yao mbalimbali ikiwemo suala la huduma za afya,Barabara,Maji sambamba
na tatizo sugu la zao la Korosho wilayani humo.
Post a Comment