Home » » Lema amshtaki Sadifa kwa Spika akidai kumkashifu

Lema amshtaki Sadifa kwa Spika akidai kumkashifu

Written By JAK on Friday, November 15, 2013 | 5:13 AM

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2011/03/Lema.jpg
Lema alisema picha hizo zimeanza kusambazwa tangu mwezi uliopita kwenye Mtandao wa Fikra Huru.

Na Mussa Juma, Mwananchi

Kwa ufupi
    Akizungumza mjini hapa jana, Lema alisema picha hizo zimeanza kusambazwa tangu mwezi uliopita kwenye Mtandao wa Fikra Huru.


Mke wake, Godbless Lema, Neema anasema anaamini ukweli wa picha hizo chafu utajulikana.

Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameomba Bunge kuingilia kati kuchunguza na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, watu waliotengeneza  picha zinazomkashifu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya jamii.

Akizungumza mjini hapa jana, Lema alisema picha hizo zimeanza kusambazwa tangu mwezi uliopita kwenye Mtandao wa Fikra Huru.

“Tayari nimemwonyesha picha hizi  Spika Anne Makinda na Katibu wa Bunge, wakanielekeza niandike barua uchunguzi uanze na nimeandika barua tangu Novemba 11,” alisema Lema na kuongeza:

“Binafsi nina watu wangu, tumefuatilia na kubaini wanaoendesha mchezo huu ni baadhi ya  vijana wa Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM), akiwamo mwenyekiti wake, Sadifa Juma Hamis na kada wa chama hicho, Mtela Mwampamba.”

Hata hivyo, Mwampamba alimshangaa Lema kumhusisha na utengenezaji picha hizo na kumshauri kwenda mahakamani kama ana ushahidi.

 “Namwambia aache woga, kila siku anapohubiri hakuna dhambi kubwa  kama woga, sasa kwa nini  anakuwa mwoga, Lema afanye siasa zenye tija mbona anajiita kamanda, kamanda gani anakuwa mwoga aende mahakamani,” alisema.

Naye  Sadifa alikanusha kuhusika na utengezaji wa picha hizo na kwamba, hana sababu ya kufanya hivyo kwani hana tatizo lolote na Lema.

“Natokea Zanzibar, yeye anatoka Arusha sasa kwa nini nifanye hivyo wakati sina  tatizo lolote na yeye, hili suala lenyewe ndiyo nalisikia leo,” alisema Sadifa na kuongeza:

Lema alidai mwenyekiti huyo alikuwa akisambaza picha hizo bungeni, akiwaonyesha wabunge mbalimbali hatua ambayo ilimsababisha kupeleka malalamiko kwa Katibu wa Bunge na Spika.

Alisema alitaka kumvamia Sadifa akiwa bungeni kumpokonya simu yake aliyokuwa akitumia kusambaza picha hizo, lakini alizuiwa na Spika na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger