Home » » Mwakyembe atangaza vita

Mwakyembe atangaza vita

Written By JAK on Friday, November 15, 2013 | 5:19 AM

http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/Mwakyembe.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.PICHA|MAKTABA

Na Burhani Yakub, Mwananchi

Kwa ufupi
Dk Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi na kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani hapa, alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA, polisi, TPA na wafanyabiashara.


Tanga.Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza vita rasmi na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu mkoani Tanga na maofisa wa vyombo vya Serikali waliopo kwenye mtandao huo.

Dk Mwakyembe aliwataka watambue kuwa, kiama chao kimefika kwa sababu tayari Serikali inayo majina ya wafanyabiashara na baadhi ya maofisa wa polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wanaotumika kufanikisha upitishaji magendo.

Dk Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi na kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani hapa, alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA, polisi, TPA na wafanyabiashara.

Alisema baada ya Serikali kudhibiti Bandari ya Dar es Salaam, wafanyabiashara magwiji wa upitishaji bidhaa za magendo wamehamishia nguvu zao Tanga.

“Natangaza rasmi vita dhidi ya walio katika mtandao huo, watambue hatuwezi kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari bubu na mpaka wa Horohoro kuwa gulio la walanguzi, wapitishaji dawa za kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger