Home » » IGP MSTAAFU SAID MWEMA AAGWA RASMI POLISI BARRACKS, LEO JIJINI DAR

IGP MSTAAFU SAID MWEMA AAGWA RASMI POLISI BARRACKS, LEO JIJINI DAR

Written By JAK on Saturday, February 15, 2014 | 9:51 PM

 IGP Mstaafu, Said Mwema akipokea Salaam ya heshima na utii iliyotolewa na Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi(hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 15, 2014 katika Viwanja vya Polisi barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu, Said Mwema akikagua Gwaride Maalum alililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria.
 Gadi ya Wanaume iliyoundwa  na Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakipita kikakamavu mbele ya IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo pichani) kwa mwendo wa haraka katika hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa Sheria.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi ambao walijitokeza kwa wingi katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi IGP Mstaafu kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa Sheria. Sherehe hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barrack Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu Said Mwema akiwa katika Gari Maalum la wazi huku akipunga mikono kwa Maafisa, Askari, Wageni Waalikwa na Wananchi mbalimbali katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipunga mikono wakati IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi. Hafla hiyo fupi imefanyika kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma(wa Nne toka kulia) ni Mkrugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid(tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile).
 Wanakikundi rafiki wa Ulinzi Shirikishi wakipiga makofi wakati IGP Mstaafu Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. IGP Mstaafu Said Mwema atakumbukwa hapa Nchini kwa namna alivyoshirikiana na Wananchi pamoja na Wadau wa Amani katika dhanaya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii.
 IGP Mstaafu Said Mwema(kushoto) akimkabidhi kitara IGP Mpya wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu(kulia) ikiwa ni ishara ya Makabidhiano ya Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Polisi hapa Nchini. Sherehe hizo zilizopambwa na Gwaride Maalum lililounndwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi imefana sana katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu Said Mwema(wa pili kushoto) akipongezwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja baada ya hafla fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria. Hafla hiyo fupi iliyofana sana imefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
IGP Mstaafu Said Mwema akiagana na Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve mara baada ya hafla fupi ya kumuaga rasmi. Hafla hiyo imefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks leo Februari 15, 2014 Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje).
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger