Home » » JK NA DK SHEIN WALIPOTUA MJINI DODOMA LEO NA KUHUDHURIA KIKAO CHA NEC

JK NA DK SHEIN WALIPOTUA MJINI DODOMA LEO NA KUHUDHURIA KIKAO CHA NEC

Written By JAK on Saturday, February 15, 2014 | 10:06 PM

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma tayari kuongoza kikao cha NEC kilichoanza jioni ya leo mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma mara tu alipowasili kwenye uwanja wa ndege mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma ya asili kutoka kikundi cha ngoma cha mkoa wa Dodoma wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma,Mwenyekiti wa CCM Taifa amewasili jioni ya leo Dodoma tayari kuongoza kikao cha NEC kitakachofanyika kwa siku mbili.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Rehema Nchimbi mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali mbali alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma leo akihudhuria katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kinachoanza jioni hii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiimba wimbo wa Chama alipokaribishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Makao Makuu Dodoma leo,mara liowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mjini (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Rehema Nchimbi.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Makao Makuu Dodoma wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma leo.(Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.)
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger