Home » » JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU RAIA WA ETHIOPIA NA MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU RAIA WA ETHIOPIA NA MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

Written By JAK on Wednesday, February 19, 2014 | 10:03 PM

 Watu  waliokamatwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria
 Afisa uhamiaji mkoa wa Dodoma Ally Haji Amil 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP David Misime.
Habari na Sylvester Onesmo, picha
na Peter Simoni wa Jeshi la Polisi Dodoma.
----------------
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wanne raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria, watu hao walikamatwa kufuatia taarifa ya raia wema waliokuwa wakisafiri nao katika basi hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma DAVID MISIME – SACP amesema wahamiaji hao wamekamatwa tarehe 18/02/2014 majira ya 16:00hrs huko eneo la Kisasa barabara Kuu ya Dodoma – Morogoro Manispaa ya Dodoma katika basi la Kampuni ya SIMIYU EXPRESS lenye namba za usajili T.892 AQY SCANIA lililokuwa likiendeshwa na ATHMAN S/O SELEMAN, 40yrs, kabila Mpare, Islam, mkazi wa Shekilango Dar es Salaam likitokea Mwanza kuelekea Dar es salaam.
Aidha raia hao hawakuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili wala Kiingereza bali lugha yao ya Kihabeshi, lakini pia  walikutwa na tiketi za kusafiria zenye majina tofauti ambayo sio majina yao halali ambayo ni EMAMU, MARWA, CHACHA na JOSEPH. 

Baada ya kukamatwa basi lilifikishwa kituo cha Polisi kati na kufanyiwa upekuzi wa kina, kuhoji baadhi ya mashahidi ambao ni abiria waliokuwa katika basi hilo ambapo uchunguzi wa awali ulibaini kuwa,wahamiaji hao wanafahamika kwa majina ya:  
1.  MISGHANEA DETAMO,
2.  MAKESO WILDEMKEL,
3.  GERZAN WOLDISMATI,
4.  TIMULO WOLEPO,
Kondakta wa basi aitwaye HASHIM s/o JUMA, 29yrs, Mwarabu, Islamu, mkazi wa Magomeni Dar es Salaam naye anashikiliwa kwa mahujiano kuhusiana na watu hao. 
Wakati huo huo watu wawili raia wa Malawi nao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuishi nchini bila kibali, raia hao walitambulika kwa majina ya DENIS S/O MANDA, miaka38, Mndali na RICHARD S/O PILI, miaka 25, Mchewa wote walikuwa wakiishi Ipagala Mkoani Dodoma. Jumla ya watuhumiwa nane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo. 
Kwa upande wake Afisa uhamiaji mkoa wa Dodoma ALLY HAJI AMIL amesema wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya doria kwenye nyumba za kulala wageni na misako katika vyombo vya kusafiria ili kupambana na wahamiaji haramu hasa katika kipindi hiki ambacho bunge la Katiba linaendelea mkoani hapa.
Kamanda MISIME amewaomba wakazi wa Dodoma kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa haraka iwezekanavyo wanapogundua kuwepo kwa tukio lolote la uvunjifu wa sheria. Pia uchunguzi zaidi kubaini mtandandao wa mawakala wa usafirishaji wa wahamiaji haramu unaendelea. 
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger