Home » » MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

Written By JAK on Thursday, February 13, 2014 | 12:31 AM

 Mwalimu Vitus Lawa akikabidhi fomu ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kalenga kwa Katibu wa Wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga mjini Iringa.
 Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na waandishi baada ya kurudisha fomu za kuwania kuchaguliwa kuwania ubunge wa jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga. (Picha zote na Denis Mlowe)
Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
========  ======  ========
MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

Na Denis Mlowe,Iringa

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngwelo iliyoko Lushoto mkoani Tanga, Vitus Lawa (41) amejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akitumia msemo wa neno ‘Jembe ambao kila herufi imebeba maana ya ujumbe, Lawa aliyesindikizwa na baadhi ya wanachama wa Chadema wa kata ya Kalenga alilirudisha fomu za Chadema kwa kuwapa moyo wakazi wa Kalenga kuwa mkombozi wa kweli amefika katika kuwaletea maendeleo.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kurudishafomu  mbele ya Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo, Lawa alisema uwezo wa kuwakomboa na kuwaletea maendeleo wakazi wa Kalenga umefika hivyo ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo katika kushirikiana na kushikamana katika kuleta maendeleo.

Alisema endapo atapatiwa nafasi atatumia ajenda tano ambazo zinamaana ya neno jembe, imebeba maana kubwa sana katika maisha ya binadamu kwa uwezo wangu wa akili na ubunifu,neno hilo lina maana ya jamii bora ambayo itatokana na kuwajengea uwezo kwa wajasiliamali wote na elimu bora pia inawezekana kwa wakazi wa Kalenga kwa kusimamia upatikanaji elimu iliyobora kwa taasisi husika na wadau wake.

Lawa alisema endapo chama kitampitisha kuwania ubunge kwa jimbo la Kalenga atawaletea maendeleo  wakazi hao kwa kuhakikisha miundo mbinu inakuwa bora kwa wilaya hiyo kwa kuanzisha shirika la wakandarasi ambao watasimamia kitengo hicho.

Aliongeza kuwa kuwainua wafanyabiashara wa jimbo la Kalenga kupitia mafunzo ya ujasiliamali na kuanzisha shirika la wafanyabiashara wa kalenga walioko nje na ndani ya mkoa wa Iringa.

“Nitaakikisha naanzisha kundi la wana Kalenga waishio ndani na nje ya mkoa kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya jimbo kwa mtindo wa egima hivyo najiamini nina uwezo wa kuwasaidia wananchi wa Kalenga na siasa safi kwa wananchi ni JEMBE” alisema Lawa

Hadi sasa kuna wanachama  13 wa Chadema wamejitokeza katika ofisi za chama hicho wilaya ya Iringa vijijini kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Kalenga katika Uchaguzi mdogo wa kujaza kiti hicho kilichoachwa wazi na Dk William Mgimwa aliyefariki Januari 1, mwaka huu, utafanyika Machi 16, mwaka huu.

Wananachama wengine waliojitokeza  kuomba kugombea nafasi hiyo kuwa ni pamoja na Lawa ni Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema Makoga, Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, Mussa Mdede, Mchungaji Samweli Nyakunga,  Daniel Luvanga na Anicent Sambala.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger