Home » » WAZIRI MAGHEMBE ATAMBELEA MIRADI YA MAJI MKOA WA PWANI

WAZIRI MAGHEMBE ATAMBELEA MIRADI YA MAJI MKOA WA PWANI

Written By JAK on Wednesday, February 12, 2014 | 11:53 PM

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimuonesha Waziri wa Maji, Profesa Maghembe samaki waliokufa katika bwawa linalosadikiwa kutiwa sumu na mtu asiyejulikana.
 Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze jinsi ulivyochafuka.
Mkurugenzi wa majisafi na usafi wa mazingira Chalinze Christa Mchomba akimuonesha Waziri wa Maji Profesa Jumanne maghembe na aliyoongozana nao jinsi mto Wame ulivyochafuka, aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza.
Waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kibindu wilayani Bagamoyo. Waziri aliwahakikishia kisima cha maji katika kijiji chao.

Atoa maagizo kwa kwakurugenzi na wahandisi wa maji
        *Ajionea Maji yalivyochafuko mto Wame

Na Athumani Shariff
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, amefanya ziara Mkoani Pwani ili kukagua na kutoa maelekezo katika miradi ya maji ya Mkoani humo.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ilikagua miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya Chalinze, Visiga, Vigwaza, Kibinda na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze.
Profesa Maghembe pia alitembelea bwawa la maji la Pigo shule ilikagua na kujionea hali ya bwawa hilo lililotiwa sumu na watu wasiojulikana.
Bwawa la Pigo linasadiwa kuwa limetiwa sumu na watu wasiojulikana kutoka na maji yake kuwa na mapovu huku samaki na vyura kufa na kuonekana wakielea katika bwawa hilo.
Akiueleza msafara huo, Waziri Maghembe alisema, tayari ameshawaagiza wataalamu wa maabara ya maji kutoka Wizara ya Maji ili wakayakague maji hayo, lakini wananchi wasiyatumie maji haya.
Profesa Maghembe pia alimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira chalinze Christa Mchomba, ahakikishe watu waishio maeneo hayo hawapati mgao wa maji ili wasiende kuchota maji hayo yenye sumu.
“Mkurugenzi hakikisha wananchi hawa hawapati mgao wa maji ili wasijekuchota maji haya” alisisitiza Waziri Maghembe.
Pamoja na miradi hiyo, Waziri pia alitembelea na kujionea jinsi mto Wame ulivyochafuka. Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze umechafuka kutoka na shughuli za kibinaadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vyake vya Mkoani Morogoro.
Akieleza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze, Christa Mchomba alisema “Mto Wame umechafuka sana hali ambayo haijawahi kutokea tangu kuanza kwa mamlaka hii ya maji ya Chalinze. Maji yamekuwa tope kutokana na shughuli za kibinaadamu zinazofanywa hasa katika vyanzo vya Morogoro.
Kutokana na uchafuzi huo uliopelekea maji kuwa tope uzalishaji wa maji umepungua hadi kufikia asilimia 8 kitu ambacho kimepelekea mgao wa maji katika maeneo mengi yaliyokuwa yakipata huduma ya maji kupitia mamlaka hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, alimshukuru Waziri wa Maji kwa kutenga muda wake ili kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Bagamoyo.
“Kwa niaba ya wananchi wa Bagamoyo, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kwakutenga muda wako kuja kututembelea na kujionea miradi ya maji katika Halmashauri yetu. 

Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger