
Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Halamshauri ya mji mdogo wa Namanyere Wialayani Nkasi jioni ya leo,kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa Ofisi za chama hicho.Kinana alieleza kuwa kufuatia na taarifa mbalimbali alizokabidhiwa na Viongozi wa chama wilayani humo,alieleza kuwa wilaya ya Nkasi ina kero kadhaaa ikiwemo suala la Maji,Umeme,Uhaba wa walimu,Barabara pamoja na tatizo la soko la kuuza mazao ya wakulima,Kinana ameahidi yote hayao kuyafannyia kazi kwa kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa namna moja ama nyingine.

Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakisikiliza kwa makini huku na wao wakiandika mambo kadhaa yaliyokuwa yakizungumza na Kinana kwa ajli ya kuweka kumbukumbu.

Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Rukwa,Ndugu Hypolitus Matete akimtambulisha Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa,kutoka Zanzibar,Balozi Ali Abeid karume kwa wananchi halmashauri ya mji mdogo Namanyere,wilayani Nkasi mkoani Rukwa,kwenye mkutano wa hadhara.

Wanachama mbalimbali wa CCM na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa
hadhara,wakishangilia jambo.Ambapo katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa halmashauri ya mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa jioni ya leo.

Baadhi ya wananchi wakishangilia jambo.
PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA.

Post a Comment