Ridhiwani akiteta jambo na Mariam Khami ambaye ni mlemavu wa macho katika Kijiji cha Kifulete baada ya kumaliza mkutano wa kampeni leo
Diwani wa Kata ya Kimange, Hussein Hading'oka akiangua kilio mbele ya wananchi na mgombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Ridhiwani Kikwete baada ya kukerwa na kitendo cha mkandarasi wa maji kuchelewesha Mradi wa maji katika kata hiyo. Tukio hilo lililtokea akielezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Kiona leo.
Diwani Hading'oka akifutwa machozi na mmoja wa wanakijiji cha Pongwe Kiona leo.
Ridhiwani (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto pamoja na mmiliki wa Blogu ya Wananchi, William Malecela wakati wa kampeni za jimbo la Chalinze ambapo Ridhiwani anagombea.
Ridhiwani akijadiliana jambo na Pinto katika Kijiji chA Kimanga leo.
Kwaya ya Kijiji cha Kimange, Kata ya Kimange wakitumbuiza kwa furaha wakati wa kampeni za CCM Jimbo la Chalinze.
Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiungana na wananchi wa Kijiji cha Pongwe Kiona kumuombea aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Chalinze, marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mkutanio wa kampeni leo.
Mzee Omari Abdallah (80) akimsikiliza kwa makini mgombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM,Ridhiwani Kikwete aliyekuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Kiona leo.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya vijana wa Kijiji cjha Pongwe Mnazi baada ya kumalizika kwa mkutano kijijini hapo leo.
Ridhiwani akisalimiana na baadhi ya wazee katika Kijiji cha Kifulete, Kata ya Kimange.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akijadiliana jambo na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Changarika leo.
Wasanii wa ngoma ya Sero wakicheza mbekle ya Ridhiwani Kikwete wakati wa Mkutano wa Kampeni katika Kijiji cha Changarika , Katea ya Mbwewe leo.

Post a Comment