Home » » Polisi Mtwara yakamata kilo 222 za meno ya Tembo

Polisi Mtwara yakamata kilo 222 za meno ya Tembo

Written By JAK on Thursday, October 31, 2013 | 10:12 AM



Na.Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.


JESHI Polisi Mkoani Mtwara  limefanikiwa kukamata  gari lenye namba za usajili T.867 aina ya Toyota Carina Saloon likiwa limebeba  shehena ya mifuko  yenye meno ya Tembo tisini (90)  yenye uzito wa kilogramu 222.1 ya thamani  zaidi ya  shilingi bilioni moja (1,082, 025,000/=)



Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Steven alisema kuwa gari lilikamatwa Kata ya Maendeleo, wilaya ya Masasi katika barabara kuu ya Tunduru kuelekea Masasi.



Zelothe alisema kuwa askari wa doria walilitilia shaka gari hilo na kumuamuru dereva  kusimama kuonyesha leseni  ya udereva  ambapo dereva wa gari hilo hakuwa nayo, ndipo askari alichukua hatua yakufanya ukaguzi ambapo alikuta gari hilo limejaza shehena ya mifuko inayosadikiwa kuwa ni meno ya Tembo.



 “Askari waliamua kulifisha gari hilo kwenye kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Masasi umbali wa kilometa moja kutoka sehemu lilipokamatwa gari hilo, wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni dereva na mwenzake walikuwa wakimshawishi askari huyo waelewane ili wampatie shilingi milioni tatuaweze kuwaachia lakini askari huyo alikataa na kufanikiwa kulifikisha gari hiyo kituoni” Alisema Zelothe.



Alisema kuwa kabla gari hilo halijasimama vizuri dereva na mwenzake waliruka na  kutokomea vichochoroni, juhudi za kuwasaka bado zinaendelea ili waweze kukamatwa na  kufikishwa mahakamani.



Miongoni mwa vitu vilivyokutwa ndani ya gari hilo wakati wa upekuzi ni pamoja na simu moja ya kiganjani aina ya Techno, mizani aina ya tonash, fomu za “notification” pamoja 
na Bank slip.



Kutokana na uchunguzi uliofanyika imebainika kuwa dereva wa gari hilo anatajwa  kuwa ni Oliver Lucas mkazi wa Masasi na mwenzake aliyekuwa naye bado  hajatambulika na inaaminika kuwa tajili wao ni mtu mwenye jina la Hassan Koko anayejulikana kwa jina 
maarufu la   Twalib Nyoni.





Kamanda Zelothe amewataka wananchi kuongeza kasi ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuwezakukomesha biashara hii haramu 
ya usafirishaji wa nyara za Serikali na kutoa taarifa 
itakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ili waweze 
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Na Michuzi Blog
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger