Home » » Arsenal, Chelsea mdomoni kwa Wajerumani leo

Arsenal, Chelsea mdomoni kwa Wajerumani leo

Written By JAK on Wednesday, November 6, 2013 | 11:45 AM




Paris, Ufaransa. Atletico Madrid imekuwa katika mafanikio makubwa Hispania na Ulaya watapata zawadi yao ya kwanza leo kama watashinda dhidi ya Austria Vienna jijini Madrid na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

Vumbi jingine litatimuka kwa kuwashusha vinara wa England, Arsenal na mahasimu wake Chelsea wakionyesha kazi na miamba ya Bundesliga, Borussia Dortmund na Schalke 04.

Chelsea  v Schalke 04

Chelsea wataikaribisha Schalke siku chache baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Newcastle, kipigo hicho kilimfanya Kocha Jose Mourinho kudai alifanya makosa  11. “Tupo katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, lakini kama tutafungwa tena basi tutajiweka kwenye hali ngumu,” alitadharisha Mourinho.

Basel  v Steaua Bucharest

Basel wanawakaribisha Bucharest wakiwa na rekodi mbaya ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza hivyo sasa wanapigana kuhakikisha wanapata tiketi ya kucheza Europa Ligi.

Borussia Dortmund  v Arsenal Dortmund iliiharibu sherehe ya kuzaliwa Arsene Wenger alipokuwa akitimiza miaka 64, waliposhinda 2-1 kwenye Uwanja wa Emirates. Dortmund wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi katika Bundesliga walipoichakaza Vfb Stuttgart  6-1. Arsenal wenyewe walishinda 2-0 dhidi ya Liverpool.

Napoli v Marseille

Rafael Benitez ameiongoza Napoli kushinda mechi tatu mfululizo za Serie A, na leo atakuwa mwenyeji wa Marseille ambao aliwafunga 2-1 kwenye mchezo uliopita. Matokeo hayo yameifanya timu hiyo ya Italia kuwa na matumaini ya kufuzu kwa mtoano, akiwa sawa kwa pointi sita na Dortmund na Arsenal, huku Marseille wakiwa hawana pointi yoyote.

Zenit St Petersburg  v FC Porto Zenit wataiacha zaidi Porto katika harakati za kusaka kufuzu kama watashinda leo na kufanya tofauti kati yao kuwa pointi nne ikiwa wamekiza mechi mbili. Zenit walifanya kazi ya ziada kuwafunga Porto kwenye mchezo uliopita walikutana hivyo kuifanya mechi ya leo kuwa na utamu wa aina yake.

Atletico Madrid  v Austria Vienna Atletico imetumia vizuri udhaifu wa kundi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16 bora kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2008/09. Pia ushindi wa Atletico utawafanya waweke rekodi ya kushinda mechi nne mfululizo za michuano hiyo mikubwa ya Ulaya, wakivunja rekodi yao ya kushinda mechi tatu msimu wa1958/59.

Ajax  v Celtic Ajax inahitaji japo pointi moja ili kujiweka katika matumaini hata ya kupata nafasi ya tatu ya kucheza Europa Ligi. Celtic wenyewe watakuwa wakisaka ushindi mwingine dhidi ya Wadachi hao ili kufufua matumaini ya kucheza hatua ya mtoano kwa mara ya pili mfululizo.

Barcelona  v AC Milan Barcelona bado haijawa katika kiwango chake cha juu, lakini inayo nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora wakati watakapowavaa wachovu AC Milan wanaondamwa majeruhi.

Shaka ya Barcelona ni ndogo kulianganisha na Milan ambao wameanza msimu wa Serie A vibaya zaidi baada ya miaka 20 kupitia. Kama Milan watafungwa na Barcelona na Celtic watashinda basi nafasi yao ya kusonga mbele itakuwa finyu zaidi.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger