Home » » Mikoa ya Puntland, Somaliland inapepesuka kutoka mvua za baada ya kimbunga, mafuriko

Mikoa ya Puntland, Somaliland inapepesuka kutoka mvua za baada ya kimbunga, mafuriko

Written By JAK on Monday, November 18, 2013 | 6:51 AM


Wasomali wakimuokoa ngamia baada ya mafuriko ya majanga kukipiga kijiji cha Sin Ujiif katika mkoa wa Somalia wa Puntland hapo tarehe 13 Novemba. 
Mvua kubwa iliyofuatiwa na kimbunga, ambayo ilipiga mkoa wa Somallia wa Puntland na kusababisha vifo vya watu 300, pia ilileta mafuriko katika sehemu za mkoa wa Somaliland na kusababisha hasara kubwa katika mji wa bandari wa Berbera.Katika Puntland hadi kufikia Jumatano (tarehe 13 Novemba), idadi ya vifo vya watu kutokana na kimbunga hicho ilithibitishwa kufikia 143, Waziri wa Nchi Wa Utawala Bora Mohamed Farah Isse aliiambia Sabahi. Serikali ya eneo hilo ilisema watu wapatao 300 walihofiwa kuwa wamekufa na mamia ya wengine hawajulikani walipo.Kiasi cha wanyama 100,000 -- wengi wao wakiwa mbuzi-- walipotea katika kimbunga hicho, sse alisema.

"Mvua hiyo imeambatana na baridi kali sana, upepo na maji mengi, ambao umeua watu na wanyama," alisema. "Hatuwezi kuyafikia maeneo yaliyoathirika kwa sababu magari yanakwamba katika matope. Tulitoa kiasi kidogo cha msaada kwa wilaya ya Dangorayo, hata hivyo, hatuwezi kufikia Eyl na Bandarbeyla."

Mwonekano wa Kimbunga cha Tropikana 03A kutoka chombo cha angani wakati kikipita kaskazini ya Somalia hapo tarehe 10-11- 2013. [Na PICHA YA AFP/NASA/KITINI]

Baraza la mawaziri la Puntland limeteua kamati ya mashirika -- iliyoundwa na masuala ya ndani ya mkoa, wizara za afya na mipango, pamoja na mashirika ya kushughulikia maafa -- kusimamia mwitikio wa kibinadamu kutokana na mgogoro huo na kimbunga, Isse alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Garmal Gurey, Salad Qayad alisema kwamba kimbunga hicho kiliua watu 25 katika kijiji chake pekee, kilichoko kilomita 80 mashariki ya Dangorayo katika mkoa wa Nugaal wa Puntland.

"Watu waliofatiki ni pamoja na mama mmoja na watoto wake sita, wakati baba na mpwa wake tu ndio waliookoka katika familia," Qayad aliiambia Sabahi, na kuongeza kwamba kijiji hicho kimekuwa kama kisiwa kilichozungukwa na maji pande zote.

Mvua ziliipiga Berbera mfululizo, ikisomba madaraja na kuharibu majumba vibaya sana. Juu, wakaazi wakitathmini hasara hapo tarehe 14 Novemba. [Na Barkhad Dahir/Sabahi]

Watu wanaoishi katika maeneo ya Puntland yaliyokumbwa na kimbunga pia walieleza hofu yao kwamba watu wengi zaidi wanaweza kufa kutokana na tishio la kulipuka kwa magonjwa.

Katika eneo la Karkaar la Puntland, kuna majeruhi wengi na watu wagonjwa ambao wanahitaji huduma za afya kwa haraka, alisema Ahmed Mohamud Hassan, mkuu wa tiba katika kijiji cha Kulule. Chakula kidogo kilichobakia kijijini kilikuwa kinamalizika, alisema.

"Hapa kijijini kuna watu 1,000 waliokwama ambao wanyama wao wamekufa na hawana chakula," aliiambia Sabahi.

Mifugo iliyouliwa wakati wa kimbunga huko Eyl, Puntland, tarehe 13 Novemba. [Na Abdi Moalim/Sabahi]

Hassan alisema aliishukuru serikali ya shirikisho kwa kuahidi msaada wa dola milioni moja kwa msaada wa baada ya kimbunga, lakini alitoa wito kwa maofisa kuwasilisha msaada huo.

"Ikiwa msaada huo utachelewa, hautatufaa kwa lolote," alisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Somaliland Mohamed Bihi Yonis na Waziri wake wa Mambo ya Ndani Ali Mohamed Waranadde walisema siku ya Jumanne (tarehe 12 Novemba) kwamba mkoa huo pia utashiriki katika juhudi za msaada wa kibinadamu kwa wahanga wa kimbunga wa Puntland.

Kimbunga kilichoambatana na uharibifu
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger