Home » » WACHINA MENO YA TEMBO WACHUNGUZWA

WACHINA MENO YA TEMBO WACHUNGUZWA

Written By JAK on Monday, November 4, 2013 | 11:21 AM



Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Kwa ufupi
 Wakati Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku akisisitiza kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya raia wa China kukamatwa na vipande 706 vya meno ya tembo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) Eliezer Feleshi amesema wanasubiri uchunguzi wa suala hilo kukamilika.

Wakati Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku akisisitiza kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

“Unajua ile ni ‘task force’ iliyoanzishwa na waziri mwenyewe, na amelizungumzia, sasa mimi siwezi kusema kilichokwishazungumzwa na waziri,” alisema Kamanda Kova. Juzi Kagasheki aliongoza operesheni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na ujangili katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni sambamba na polisi na maofisa usalama na kufanikiwa kuwakamata raia watatu wa China, Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wakiwa na meno hayo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Feleshi alisema kazi yake ni kupambana na uhalifu na kufafanua kuwa uchunguzi ukikamilika, taratibu za kufikishwa mahakamani zitafanyika.

“Tunasubiri uchunguzi ukamilike kwanza, kisha taratibu zingne zitafuta kwa mujibu wa sheria,” alisema Feleshi.

Meno hiyo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger