Home » » NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Written By JAK on Wednesday, February 5, 2014 | 2:05 AM

IMG_0979 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke. IMG_1007 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akizungumza na wakazi wa eneo la mradi wa kisima cha maji cha Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya ya Temeke, kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Barabara ya Mwinyi, Yahya Mnali. IMG_1011 
Wakazi wa eneo la mradi wa kisima cha maji Kichapwi, kata ya Kilakala, wilaya ya Temeke, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala (hayupo pichani). Mradi wa kisima cha maji Tabata Segerea. IMG_1048 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akifungua maji ya mradi wa kisima cha maji, Chang’ombe Unubini, wilaya ya Temeke.
……………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, leo ameendelea na ziara yake ya jijini Dar es Salaam kwa kukagua miradi ya visima vya maji inayosimamiwa na DAWASA maeneo ya Temeke na Segerea.
Mhe. Makala aliweza kufika kwenye miradi ya visima vya maji maeneo ya Chang’ombe Unubini, Kichapwi na Segerea na kuona namna miradi hii ilivyosaidia kutatua kwa kiasi kikubwa cha tatizo la maji katika maeneo hayo ya jiji.
Naibu Waziri aliridhika namna miradi hiyo ya kijamii, ambapo Serikali ikishirikiana na wananchi wameweza kutekeleza mpango wa Serikali kuhakikikisha inaleta ahueni kwa kutoa huduma za kuridhisha za maji kufikia mwaka 2015.
“Napenda kuwashukuru wananchi na DAWASA kwa kazi nzuri iliyofanyika katika miradi hii, na ni dhahiri kuwa mpango wa kutoa huduma nzuri ya maji jijini Dar es Salaam na nchi nzima inaendelea vizuri. Ningependa kuwaasa wananchi wazidi kushirikiana kwa ukaribu na Serikali ili kuhakikisha miradi hii inatunzwa na kuendelea kupanuka zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wenyewe na nchi nzima kwa ujumla”.
Vile vile Mhe. Makala aliipongeza Kamati ya Jumuiya ya Watumia Maji ya Mradi wa Kichapwi, Kilakala, wilaya ya Temeke kwa uendeshaji mzuri wa mradi huo na kuweza kukusanya pesa nyingi, kiasi cha sh. Mil 11. Huku wakifanikiwa kufungua akaunti mbili za benki kwa ajili ya makusanyo ya mapato na rasilimali kama walivyoagizwa na DAWASA.
“Pamoja na uchanga wake, Kamati ya Maji ya Kichapwi imefanya vizuri sana katika kutekeleza majukumu yake na hakika ni mfano wa kuigwa nchini na kwa kweli wanastahili pongezi nyingi”, alisema Naibu Waziri.
Mhe. Makala atamaliza ziara yake ya siku tano jijini Dar es Salaam kesho, kwa kutembelea maeneo ya Ubungo, na baada hapo kwenda Morogoro kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mkoani humo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger