Home » » Dr JAKAYA KIKWETE KATIKA PANTONI, KUHANI KIFO CHA KADA WA CCM

Dr JAKAYA KIKWETE KATIKA PANTONI, KUHANI KIFO CHA KADA WA CCM

Written By JAK on Thursday, April 17, 2014 | 11:05 PM


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la  awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasala awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na na baadaye kutelemka na Rais aliyekuwa akielekea kuhani msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika Kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger