Powered by Blogger.

Ads 468x60px

Social Icons

NEWS

Featured Posts

Latest Post

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI

Written By JAK on Wednesday, October 30, 2013 | 7:50 AM



YA ASKOFU MSTAAFU, MHASHAM RAYMOND MWANYIKA ILIYOFANYIKA MKOANI NJOMBE .
 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika Anne Makinda na viongozi wengine wakitoa heshima za mwisho na kuaga  mwili wa marehemu
 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya Askofu Mstaafu, Mhasham Raymond Mwanyika, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika leo katika Kanisa Katoliki Njombe.
 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika Anne Makinda na viongozi wengine wakielekea kanisani kuaga mwili wa marehemu
 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga kaburini
 
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana
 na Katibu Kiongozi Mstaafu Mhe Philemon Luhanjo baada ya mazishi hayo. Picha na OMR

MHE. MEMBE AKUTANA NA MKUU WA CHOMBO KIPYA CHA EU KUHUSU USALAMA MAJINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. Etienne de Poncins,  Mkuu wa Chombo kipya chini  ya Jumuiya ya Ulaya (EUCAP Nestor) kinachoshughulika  na utoaji mafunzo katika masuala ya Usalama  Majini kwa nchi za pembe ya Afrika. Bw. Poncins alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha rasmi ombi kwa Serikali ya Tanzania la kujiunga na Chombo hicho ambacho lengo lake kuu ni kutoa mafunzo, misaada ya kiufundi na kisheria ili kuziwezesha nchi washirika kukabiliana na matukio mbalimbali ya Uharamia na Ugaidi yanayotokea katika Bahari Kuu ikiwemo Pwani ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. 
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Cerian Sebregondi (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya Usalama Majini.  
Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Poncins akielezea utendaji kazi wa Chombo hicho cha EUCAP Nestor.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika wakimsikiliza Bw. Poncins (hayupo pichani).

Mazungumzo yakiendelea

Mhe. Sebregondi akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani)

Maafisa kazini! Kutoka kushoto ni Bi. Zulekha Fundi na Bw. Frank Mhina, Maafisa Mambo ya Nje wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani).

Mhe. Membe akisisitiza jambo kwa Mhe. Sebregondi na Bw. Poncins baada ya kumaliza mazungumzo yao
   
Picha ya pamoja.

WANAHABARI IRINGA WALIBANA GAZETI LA RAI

WATAKA LITAJE MAJINA YA WAANDISHI WALIOHONGWA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA IRINGA

 Mwenyekiti  wa chama  cha  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa Frank Leonard kulia akitoa msimamo  wa  wanahabari dhidi ya  gazeti la Rai na mbunge Msigwa  leo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin

 Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi  wa New habari {2006} Ltd  wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai  na Bingwa mkoa  wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati  wa kikao  cha  cha wanahabari  mkoa  wa Iringa  leo  kujadili habari  zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili 



Na  Francis Godwin Blog


WANAHABARI  mkoani Iringa wamekanusha  vikali habari  zilizoandika na gazeti la Rai  toleo namba 1067 la  jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari  mjini Iringa  wamehongwa fedha na  viongozi  wa CCM mkoa  wa Iringa ili  wasiandike habari ya msaidizi  wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga kukamatwa  kwa  tuhuma  za kujihusisha na ujangili.

Wahanabari  hao  katika  kikao  chao kilichofanyika   leo  katika  ofisi  za klabu ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) mbali ya  kukanusha habari  hizo  kuwa zimeandikwa kwa  lengo la  kuchafua  tasnia ya habari mkoa  wa Iringa ila bado wanalitaka  gazeti  la Rai  na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  kuwataja  waandishi  waliohongwa na  viongozi  wa CCM mkoa  wa Iringa kabla ya  wanahabari  hao  hawajachukua  hatua zaidi  dhidi ya gazeti  la rai pamoja na mbunge Msigwa.

"Kilichoandikwa na  gazeti la  Rai jumapili kuhusu wanahabari Iringa hawajatutendea  haki na  wametuvunjia  heshima  yetu kwa  wadau  wa habari mkoa  wa Iringa na nje ya  mkoa  wa Iringa.....ila tunachotaka Rai kuwataja  waandishi  hao  waliohongwa  ili sisi kwa  sisi kama  wanahabari  kuanza  kuchukuliana  hatua ....wakishindwa  kufanya  hivyo ndani ya  siku 14  kuanzia  leo jumanne  tutawafikisha  baraza la habari Tanzania (MCT)"

Walisema  wanahabari hao  katika tamko  lao  la pamoja  lililotolewa na mwenyekiti wa IPC Frank  Leonard  kuwa taarifa  hiyo  imechafua  vibaya  wanahabari  Iringa na  sio wacache ni  wote  kutokana na jinsi  ambavyo gazeti  hilo lilivyoandika habari hiyo tena mbaya  zaidi mwandishi  wa habari  hiyo hakuweza kuwatendea haki  wanahabari Iringa hata  kwa kuonyesha  kuwahoji katika habari  yake hiyo.

Leonard alisema  kuwa si  kweli kama  wanahabari Iringa walishindwa  kuandika habari hiyo ya  kukamatwa kwa Malenga isipo  kuwa wanahabari  Iringa ni makini na hawakutaka kuandika habari kwa  kukurupuka hivyo walitaka  kabla ya  kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi  hicho cha kupambana na ujangili  ili kulizungumzia hilo kabla  ya  kuandika jambo  ambalo  wao kama  wanahabari  walikuwa  wakilisikia  mitaani bila  kuwa na uhakika.

Uandishi  wa habari  mzuri ni pamoja na  kuzingatia maadili  ya uandishi na  sio kuandika bila  ya  kuwa na uhakika  wa kile  unachokiandika .

Hata  hivyo alisema  kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika  gazeti hilo kama  ndio msemaji wa jambo  hilo wao kama  wanahabari watamwandikia  barua mbunge  huyo  ili kusaidia  kuwataja wanahabari  waliohongwa  pesa vinginevyo wao kama  wanahabari  wa mkoa  wa Iringa hawatamvumilia mbunge Msigwa katika  hilo .

Pia  alisema  kuwa suala  hilo kwa  sasa  ameachiwa mwanasheria  wa IPC ili  kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja  na  kuwaandikia barua Rai na mbunge Msigwa kuwataka  kuthibitisha ukweli  wa kilichoandikwa  dhidi ya  wanahabari mkoa  wa Iringa.

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA POOL YAFANYA VIZURI NCHINI MALAWI



Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
 
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
 
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi,Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto) akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mabingwa wa Afrika wa mchezo wa pool wakiwa katika picha nya pamoja.Kutoka kushoto ni Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick Nyangusi,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi Wetu, Blantyre Malawi.

MCHEZAJI wa timu ya Safari Pool Taifa, Patrick Nyangusi ameibuka Bingwa wa Afrika katika mashindano ya mchezaji mmoja mmoja(singles) wanaume yaliyojumuisha timu saba kutoka katika Nchi sita za Afrika.

Patrick Nyangusi aliupata ubingwa huo kwa kumfunga mchezaji bora wa Afrika Kusini, Vishen Jagdev 6-4,katika mchezo ambao ulisisimua wapenzi na mashabiki wengi wa mchezo huo uliofanyika katika ukumbi wa kisasa wa Roben Complex jijini Blantyre.

Nyangusi kwa ubingwa huo alizawadiwa medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alichukua mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini ambaye alizawadiwa Medali ya Silver wakati  mshindi wa tatu ni Moses Mofya kutoka Zambia ambaye alimfunga mchezaji wa Tanzania, Omary Akida, 5-3 na hivyo Moses Mofya kuzawadiwa Medali ya Fedha na nafasi ya nne ilichukuliwa na mchezaji kutoka Tanzania, Omary Akida.

Upande wa timu zilizowakilisha Nchi, Zambia waliibuka mabingwa katika mchezo ambao uliendeshwa kwa mfumo wa ligi ambapo Zambia waliongoza kwa pointi 14.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na timu kutoka Nchi ya Afrika Kusini kwa pointi 12,na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nchi ya Tanzania ambao walipata pointi 9, wakati nafasi ya nne ilibaki kwa wenyeji Malawi ambao walipata pointi 4.

Akizungumza Mkurugenzi wa mashindano ya AAPA (All Africa Pool Associations), Rick Schoenlank, alizipongeza Nchi zote zilizoshiriki mashindano hayo,pili aliwapongeza waandaaji wa mashindano kwa maandalizi mazuri na mwisho aliipongeza Tanzania kwa kutoa bingwa wa Singles kwamwaka 2013.

Nae mgeni rasmi aliyefunga mashinndano hayo, Mjumbe wa Baraza la Michezo la Nchini Malawi, Sharaf Pinto, kwa niaba ya Waziri wa michezo wa Malawi,aliipongeza pia Tanzania kwa kutoa bingwa Singles na kuwaomba Tanzania kuwa karibu na wachezaji wa Malawi ili kubadilishana uzoefu na udugu pia kwa kutembeleana na kucheza mechi za kirafiki.

Lakini pia aliwapongeza Zambia kwa kutwaa ubingwa wa timu na vilevile aliwapongeza Malawi kwa nafasi waliyopata si mbaya sana, ni nafasi ambayo inawafanya wajiandae vyema kwa mashindano yajayo.

Mwisho aliwapongeza kila Nchi kwa kuleta uwakilishi na kuwatakia safari njema ya kurejea Nchini salama mpaka mashindano mengine mwakani.

Mashindano ya mwaka huu yalijumuisha Nchi takribani 6, ambazo ni Afrika Kusini, Zambia,Tanzania,Lesotho,Namibia na wenyeji Malawi 1 na Malawi 2.

Timu ya Safari Pool ililiyokwenda Malawi ina jumla ya wachezaji 8, ambao ni Mohamed Idd, Patrick Nyangusi Festo Yohana ,Mereczedec Amadeus,Omary Akida,Abdalah Hussen ,Godfrey Swain a Nahodha Charles Vernas na viongozi watatu ambao ni Meneja wa timu Nabil Hiza,Katibu wa chama cha pool Taifa, Amos Kafwinga na Makamu Mwenyekiti, Fred Mush

Mashindano ya AAPA mwakani yanatarajiwa kufanyika Tanzania jijini 

Dar es Saalaam.

AMBASSADOR MULAMULA SHARES HER EXPERIENCE AT THE GREATLAKES WITH SULISBURY UNIVESITY STUDENTS AND FACULTY



 
 
“If there is anything wrong with conflict, it is how we respond to them” remarked Ambassador Mulamula in her keynote address at the University of Salisbury in Northern Maryland at a panel discussion on Conflict Resolution and Organizational management on Friday October 25, 2013.

Addressing students and faculty, Ambassador Mulamula shared her experience as the first
Executive Secretary of the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR) from 2006 to 2011, stating that unlike the learned Salisbury community, she doesn’t study conflicts, she “live
them”

She explained the meaning of her name “Mulamula” an arbitrator, a plant that is planted on the ground after mediation of  land dispute is concluded. She added even with such a name, she still faces, like many others, challenges that exist in managing the humanistic instinctively reaction to conflicts.

“We often respond to conflicts instinctively, therefore we miss the opportunity to harness the goods that may come out of a conflict” she said.

Linking her message with recent global changes which she explains make it more difficult for organization Executives to manage conflicts in their institutions and work places. She summed her speech outlining success in mediation and facilitation as well as challenges, in a ten action points that she believes to be helpful in managing conflicts.

Ambassador Mulamula was invited to give a keynote speech at the Salisbury University by Jacques Koko, Assistant Professor and Director of the Graduate Program of Conflict Analysis and Dispute Resolution at the Fulton School of Liberal Arts at Salisbury.

After her speech, a group of panelists from the University and the community provided some light on causes and implications of organizational conflict, and how such conflicts can be addressed constructively.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. SOSPETER MUHONGO AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA SUMBAWANGA - NAMANYERE


Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo katikati akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia kwake, Mbunge wa Nkasi Kusini Ally Kessy kushoto kwake na wazee wawili kulia na kushoto wakiwawakilisha wananchi wa Namanyere (Wilaya ya Nkasi) katika uzinduzi rami wa mradi wa umeme kutoka Sumbawanga hadi Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013. Mradi huo uliogharamiwa na Serikali ya Tanzania na kukamilika hivi karibuni una gharama ya Tsh. Bilioni 4.3 na umepitia jumla ya vijiji kumi na mbili vya njiani kabla ya kutua katika Mji huo wa Namanyere uliopo Wialayani Nkasi Mkoani Rukwa. Tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na tangu kuundwa kwa Mkoa wa Rukwa mwaka 1974 Wilaya hiyo haikuwa na umeme jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe na wananchi wa Wilaya hiyo.  
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na washirika wake katika uzinduzi huo wakibofya kitufe maalum kama ishara ya kuwasha umeme katika Mji wa Namanyere leo tarehe 28, Oktoba 2013 baada ya Wilaya hiyo kukosa huduma hiyo katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Katika uzinduzi huo Prof. Muhongo amesema Mkoa wa Rukwa umetengewa zaidi ya Tsh. bilioni 30 kwa ajili ya umeme vijijini kupitia REA, Wakala wa Umeme Vijijini ambapo jumla ya vijiji 66 katika kipindi cha miezi 20 ijayo kuanzia Novemba mwaka huu 2013 vitanufaika na mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima kuwasalimia wananchi wa Kirando katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo Mkoani Rukwa. Katika ziara yake hiyo anatembelea miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi. 
Meneja Mahusiano wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Bi. Badra Masoud akisherehesha baadhi ya mambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo uliofanyika Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa na Wilaya ya Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013 juu ya upatikanaji wa umeme katika bandari mpya inayoendelea kujengwa ya Kipili Wilayani humo. Alisema kupitia REA, Wakala wa umeme vijijini kuanzia mwezi Desemba miradi mbalimbali itaanza kufanya kazi kuweza kufikisha umeme katika maeneo tofauti Mkoani Rukwa ikiwemo bandari hiyo ya Kipili.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwa ameshikilia kinyago cha mfano wa mtoto na mmoja ya wanakikundi cha ngoma za asili cha Kanondo cha Mkoani Rukwa baada ya kufurahishwa na uchezaji wa ngoma ya kikundi hicho inayoelezea malezi bora kwa watoto. 
Waziri Muhongo katika mikutano yake na wananchi hakusita kuwainua Mameneja wa Tanesco kuelezea juu ya miradi mbalimbali ya umeme Mkoani Rukwa. Kulia ni Meneja wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Magharibi Bi. Salome Nkondola na katikati ni Meneja wa Tanesco Mikoa ya Rukwa na Katavi.
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali wa Mkoa wa Rukwa.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger