Home » » Maalim Seif atembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar

Maalim Seif atembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar

Written By JAK on Tuesday, February 11, 2014 | 8:00 PM

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Afisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Ali Ussi, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu, Mkokotoni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea skuli ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya. (picha na Salmin Said, OMKR).
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. New EAC Blog - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger